BRAND NI NINI?



Katika ulimwengu wa biashara ni lazima utasikia neno brand mara kwa mara. Je brand ni nini?

Brand ni utu na mwonekano unaotengenezwa na mwenye biashara au kampuni unaotofautisha biashara  ama kampuni yake na  zingine zinazofanya kazi kama zake. Brand ni utu wa kampuni ama biashara.

Brand inajumuisha kwanzia jina, nembo, rangi, mpangilio wa kazi na mzingira hadi tabia na hulka za watendaji wake katika kampuni ama biashara. Brand ni vile biashara au kampuni inavyo husina na wateja wake. Mara nyingi tukiongelea brand watu hudhani ni nembo na rangi za kampuni tu, lahasha hivi ni viashiria vya brand, vitu viavyoonesha brand. Ila brand ili ikamilike inahitaji viashiria vyake (brand identities) pamoja na utu (personality) wake.

Brand ni vile kampuni au biashara inavyoonekana kwa nje hadi tabia na hulka za watendaji kazi wake. Kampuni ama Biashara inapotaka kutengeneza brand yake inaanza na kutathmini ni mambo yapi inataka kutatua kwenye jamii na inataka jamii iichukuliaje. Baada ya hapo inachukua hayo maono na kuyaweka katika mpango wa kujenga na kukuza brand. 

Kwenye Kujenga brand kwanza ni muhimu kuainisha maono (vision) na mipango (goals) ya kampuni ama biashara. 

Baada ya kuwa na maono na malengo inakuwa rahisi kujua wahusika unaotarajia kuwalenga au kuwafikia na brand yako. 

Ukisha wajua walengwa wako utajua hulka zao na hivyo kutengeneza mazingira ya kampuni ama biashara kuwa ya kuwavutia na kuwafanya waweze kuhusiana na kampuni/biashara yako.

Mazingira na mandhari hayo yatakuwezesha kuchagua rangi za kampuni (brand colour) na Nembo ya kampuni (Logo) ambavyo ni viashiria vya brand.

Walengwa wa bidhaa au huduma yako ndio watakao kuwezesha wewe kujua utengeneze brand ya aina gani. Mfano unatoa huduma na walengwa wako ni vijana, kitu cha kwanza kabisa ni kutengeneza mazingira rafiki kwa vijana kwenye kampuni/biashara yako. Watendaji wako wanabidi wawe vijana au watu wenye hulka za ujana. Unaweza tengeneza programu au kujiunga kwenye programu mbalimbali ambazo vijana wanapenda kushiriki.utachagua zangi zenye hulka za ujana (vibrant colours) na baada ya hapo utatengeneza mahusiano mazuri na vijana ili wawze kutangaza brand yako. 

Jambo la muhimu sana kwenye kutengeneza brand ni mahusiano (relationship). Mahusiano ndo yanaweza kujenga au kubomoa brand. Ukiwa na mahusiano mazuri na wateja wako utaweza kujenga brand nzuri na watawea kukutangazia brand yako, huta hitaji nguvu nyingi sana utangaza na kujenga brand yako. 

Hivyo basi anza leo kutengeneza brand yako ili uweze kufanikiwa kwenye biashara ama kampuni  yako. 

  • Weka maono (vision)  na mipango (goals) sahihi
  • Tengeneza thamani na ubora (values) wa huduma au bidhaa zako.
  • Chagua nembo na rangi zinazo wasilisha thamani yako. 

Kila lakheri!

Follow me on social Media!

image by zaozaa09 on freepik

Comments

Post a Comment

Popular Posts