SABABU ZA KUKOSA UJASIRI WA KUKOPA BENKI.


Twakimu zinaonesha kuwa watanzania wengi hawaendi kukopa benki, Fursa za kukopeshwa na benki ni nyingi mno lakini watu hawaendi kukopa. Unadhani ni kwa nini?

Katika kupambanua swala hili nilianza kufikiri je benki ni kina nani?

Benki ni wafanya biashara kama walivyo wafanya bishara wengine, wanauza na kununua pesa hivyo bidhaa yao ni pesa na vitu vyenye thamani kama almasi na goldi. Hivyo kama ni wafanya biashara wanatazamia kupata faida kwenye biashara yao kama walivyo wafanyabiashara wengine. Kukopesha ni huduma wanayotoa kati ya huduma zingine nyingi walizo nazo na hivyo lazima kupata faida pia.

Je wewe mfanyabiashara upo tayari kupata hasara? Hapana! ndiyo ilivyo kwa benki pia.



Nikawa ninajaribu kutafuta sababu za watanzania wengi nikiwa mmoja wapo za kuto kwenda kukopa benki.

Katika kuuliza wengi wakasema ni kwasababu benki wanamasharti magumu, kuogopa kufilisiwa mali, benki zinatoza riba kubwa, taratibu za kupata mkopa zinamlolongo mkubwa sana nk.

Nikajaribu kupambanua mwenyewe nikapata sababu zifuatazo:
  • Wengi wetu tunabiashara ambazo si za kijasiriamali hivyo zinauwezo mkubwa wa kufa na hivyo kutukosesha ujasiri wa kukopa ili kuziendeleza.
  • Tunaenda kukopa kwa haraka bila kupanga mipango madhubuti ya jinsi ya kurudisha, na kutumia mikopo hiyo kuleta kufaida na maendeleo ya biashara, tunakopa tukiwa na tatizo tunalotaka kutatua haraka. 
  • Wengine tunatumia mikopo kwa shughuli amabazo sio za biashara na hivyo huwa vigumu kuweza kurudisha kwa wakati.
  • Biashara zetu hazina mahusiano mazuri na benki hivyo uelewa mazuri wa namna ya kushirikiana na benki ili kupata maendeleo ya wote ni mdogo.
  • Kutokuwa na mipango ya biashara inayotuwezesha kuelewa kwa undani namna biashara zetu ziliyo hivyo kupelekea kushindwa kurudhisha mikopo. 
  • Hatutaki kuanza kidogo na mtaji kidogo kuanza na kuendeleza biashara ili inapokuwa na sisi kuifahamu kwa undani zaidi. Hivyo kutaka kukopa hela kwa ajili ya mtaji ambayo ni kubwa kwa biashara tusioijua.
Ni wakati wa kubadikika jinsi tunavyo fanya biashara na mahusiano yetu na benki.

Zipo sababu nyingi zaidi. Je wewe ni nini kinakusababisha kukosa ujasiri wa kwenda kukopa benki?


Comments

Post a Comment