MAMBO UNAYOHITAJI ILI KUFANIKIWA KAMA MJASIRIAMALI.
# TASWIRA
Bila ya kuwa na picha halisi ya namna unahitaji maisha yako yawe, inakuwa vigumu kuweza kutengeneza maisha yako. Wajasiriamali waliofanikiwa wanaweza kukueleza picha halisi na kwa kina ya jinsi wanataka maisha yao yawe. Unapaswa kuwa na taswira ya namna unataka maisha yako kuwa na jinsi ujasiriamali utakuwezesha kufikia hapo.# MKAZO
Ni viruzi kujua ni nini hasa unataka katika maisha yako na kuweka makazo kufikia malengo. Ni mambo mengi sana utakutanan nayo ya kukuvunja moyo na kukurudisha nyuma. Usirudi nyuma unapokutana na changamoto, bali tafuta njia nyingine ya kukabiliana nazo.# UHODARI
Kuendesha biashara yako mwenyewe kunaweza kuhitaji sana na kukuchosha mwili sana. unapokuwa hodari kutakusaidia sana kuweza kuendeleza biashara yako. Kujua afya yako kila wakati ni vizuri sana utaepukana na kuumwa ghafla kunapoweza kupelekea kufunga biashara yako.# AFYA YA UFAHAMU
Kuendesha biashara mara nyingi huleta msongo wa mawazo (stress). Hivyo usiwe na matarajio yaliyopitiliza (usinie makuu) na usijilazimishe kufanya kila jambo (usijishinikize kupita kiasi). Jua uwezo wako na fanya mambo yaliyo ndani ya uwezo wako.# UPENDO
Ukiwa kama mfanyabiashara kuna wakati inafikia unahitaji mtu wa kumlilia, hata kama wewe ni mwanaume. Unapokuwa na mtu unayeweza kushirikiana nae katika kuyabeba mambo mbali mbali unayokutana nayo, utaweza kufurahia zaidi biashara yako.# PESA
Biashara inaweza ikachukua muda mrefu mpaka kuweza kukupatia faida nzuri na hata kukulipa vizuri. Unahitaji kuweza kusubiria wakati huo kufikia, hivyo unahitaji kuwa na pesa ya kujikimu.# UNYUMBUFU (FLEXIBILITY)
Mara nyingi unapoanza biashara unakuwa pekee yako au watu wawili, hivyo itakupasa kufanya kila kitu wewe mwenyewe kama kusafisha ofisi nk. Unahitaji kuwa tayari kufanya mambo yote yanayo hitajika.# UCHESHI
Utajikuta unafanya makosa mengi sana kwenye biashara yako, unahitaji kuwa na uwezo ya kuyacheka makosa yako, kujifunza kutokana na makosa hayo na uwezo wa kuendelea mbele kwa haraka. kuwa hivyo kutakufanya uweze kufanikiwa.# TAHADHARI
unahitaji kuwa makini sana maana kwenye biashara ni rahisi zaidi kuona fursa kuliko matishio, unahitaji kuwa mtu mwenye tahadhari na kuangalia kwa makini mambo hatarishi kwa biashara yako.#FADHILA
Unapofurahia mafanikio ya biashara yako, wekeza kwa wale waliokusaidia kupata mafanikio hayo. unaweza kufanya pati, kuwapa zawadi au kuwa fanyanyia suprise mbali mbali, ili kuhakikisha wanaendelea kuwa na wewe.Kuendesha biashara yako mwenyewe kwa uhalisia najua ni ngumu sana, unahitaji kuwa wa tofauti na kuwa na mambo hayo niliyotaja pamoja na moyo wa kufanya mambo unayotaka kufanya. Jijengee uwezo huo na utafanikiwa. KILA LA KHERI!
Comments
Post a Comment