NAMNA YA KUTUMIA MUDA WAKO VIZURI ILI KUFANIKIWA KATIKA SHUGHULI ZAKO.


Katika siku binadamu wote tumepewa muda wa masaa 24, Tutatumia muda huo kufanya mambo mbalimbali ya kila siku, shughuli za kibiashara, kulala na kula pia. Ila kuna wakati unaweza kuona kuwa wote tumepewa muda sawa wa masaa 24 ila mwingine anaweza kutimiza mipango yake na mwingine kuishia kutotimiza hata mpango mmoja.

Je siri ya wajasairmali na wafanyabiashara hao wanaoweza kutimiza mipango yao na kufanikiwa zaidi ni nini?

1: Kuandika mambo ambayo unapanga kufanya kwa siku, (your to do list).

Jambo la kwanza unalotakiwa kufanya kabla ya kuanza kazi zako za siku ni kuwa na orodha ya mambo amabayo umepanga kufanya kwa siku hiyo. Unaweza kuandika orodha hiyo usiku kabla ya kulala au asubuhi na mapema unapoamka.

Kuna namna nyingi ya kuandika orodha hiyo kama vile kwa kutumia kalaamu na karatasi au kwa kutumia application za simu au zilizopo kwenye computer. Application kama todoist inayo patikana www.todoist.com inaweza kukusidia na nyingine nyingi zipo unawaza kupata kutoka kwenye mtandao.

Unapopanga mambo yako yakufanya kwa siku pangilia kutokana na umuhimu na uhitaji wa mambo. Anza na mambo ya muhimu na yalazima kwanza. Alafu ndo yafuate mengine. Pangilia pia mambo kutokana na muda yanayohitaji, anza na mambo yanayohitaji muda mchache kwanza.

Kama upo ofisini jambo muhimu lakuzingatia: usianze siku kwa kusoma email hii hupelekea kukosa umakini ambao unahitaji ili kuzingati katika kufanya kazi zako. weka muda wakusoma na kujibu email baada ya kumaliza mambo ya muhimu na lazima kwanza.

2. Kuagiza (delegate)

Unapokuwa na jambo ambalo unaweza kumpa mtu afanye kwa kukuwakilisha na akaweza kufanya hiyo unavyohitaji tumia fursa hiyo. sio lazima kufanya kila kitu mwenyewe tumia wawakilishi, hii itakusaidia kupata muda wa kutosha kufanya mambo mengine ambayo huwezi kuwakilishwa. Na mwisho wa siku utakuwa umetimiza malengo yako.


3. Kutokupokea kila simu unayopigiwa, jumbe fupi za simu na taarifa za mitandao ya jamii.

Unapo kuwa na jambo la muhimu unafanya ni muhimu sana kuweka mkazo, lakini wakati huo huo unaweza kupigiwa simu zisizo na umuhimu, ambazo zinaweza kukuchukulia muda wako mwingi na kukuondoa fikra kwenye jambo la muhimu unalofanya. Mwisho wa siku unajikuta hukuweza kufanikisha mambo yako uliyo yapangilia. Ili kuepuka hilo unaweza kutoa sauti kwenye simu kwa muda ambao unakuwa na kazi za muhimu unafanya. Epuka kuangalia angalia simu kila unapopata taarifa za ujumbe mfupi wa simu (SMS) au kutoka kwa mitandao ya jamii.

4. Weka muda wa kufanya mazoezi (exercise).

Mazoezi ni ya muhimu sana kwa mwili wa binadamu, unapofanya mazoezi kuna homini/kemikali inatoka na kuingia kwenye damu inaitwa endorphins. kemikali hii inakufanya ujisikie vizuri na kuwa na nguvu na hamu ya kufanya kazi. Pia inakufanya kuwa mchangamfu na mwenye furaha. hali hii inakufanya uweze kufanikisha kazi zako unazo panga kufanya kwa siku. muda mzuri kufanya mazoezi ni asubuhi, hii inakufanya uwe na siku zuri na mtazamo chanya.

5. weka muda wakula chakula chenye kukupa afya (eat healthy).

Ili kuweza kuwa na mtazamo chanya na nguvu za kufanya kazi kwa bidii hakikisha unakula chakula kwa wakati na kunywa maji ya kutosha kwa siku. huwezi kuweka mkazo wa kutosha kwenye kazi kama una njaa au umeshiba sana. Epuka vyakula vinavyo kuletea gesi na tumbo kujaa, usile vyakula vizito sana ambavyo vinahitaji nguvu nyingi kumengenywa wakati wa kazi.

6. Kuwa na mtazamo chanya. (positive attitude)

Kuwa na mtazamo chanya katika kila jambo unalofanya, ondoa wazo lolote ambalo sio zuri. kila unapofanya jambo tegemea kufanikiwa, tegemea kumaliza, tegemea kufikia lengo. Amini jambo lako na mwombe Mungu akusaidie. Pata muda wa kutosha kupumzika na kulala ambao husumbuliwi na simu wala tv.

Kila lakheri

Comments

Popular Posts