BRAND NI NINI?
Katika ulimwengu wa biashara ni lazima utasikia neno brand mara kwa mara. Je brand ni nini? Brand ni utu na mwonekano unaotengenezwa na mwenye biashara au kampuni unaotofautisha biashara ama kampuni yake na zingine zinazofanya kazi kama zake. Brand ni utu wa kampuni ama biashara. Brand inajumuisha kwanzia jina, nembo, rangi, mpangilio wa kazi na mzingira hadi tabia na hulka za watendaji wake katika kampuni ama biashara. Brand ni vile biashara au kampuni inavyo husina na wateja wake. Mara nyingi tukiongelea brand watu hudhani ni nembo na rangi za kampuni tu, lahasha hivi ni viashiria vya brand, vitu viavyoonesha brand. Ila brand ili ikamilike inahitaji viashiria vyake (brand identities) pamoja na utu (personality) wake. Brand ni vile kampuni au biashara inavyoonekana kwa nje hadi tabia na hulka za watendaji kazi wake. Kampuni ama Biashara inapotaka kutengeneza brand yake inaanza na kutathmini ni mambo yapi inataka kutatua kwenye jamii na inataka jamii iichukuliaje. Baada ya h...