MAMBO MUHIMU KATIKA BIASHARA
#1 FANYA JAMBO LILILO SAHIHI KILA WAKATI
kuna wakati kwenye biashara ambapo unajikuta unahitaji kuchagua kati ya kutengeneza hela na kufanya jambo sahihi. kuna wakati utajikuta unmuuzia mtu kitu ambacho unajua hakihitaji, au unatakiwa umrudishie hela mteja amrudisha labda bidhaa kwa sababu moja au nyingine lakini unaweza kujikuta unakataa kurudishia mteja. Jambo muhimu ni kufanya jambo sahihi kwa mteja wako wakati wote kwa maana sifa yako ni ya muhimu sana katika biashara.
#2 KUWA WA TOFAUTI
katika juhudi za kutafuta masoko ni muhimu kuangalia washindani wako wanafanya nini alafu fanya wanavyo fanya lakini kwa ubora na utofauti zaidi. kufanya jambo la tofauti kwenye biashara unahitaji kuwa mwenye uthubutu, lakini thawabu yake kwenye biashara ni kubwa sana. THUBUTU KUWA WA TOFAUTI!
#3 KUWA NA WATEJA UNAOWALENGA
Je wateja wako ni kina nani? kama jibu lako ni mtu yeyote anayeweza kununua bidhaa ua huduma zako basi biashara yako iko katika hatari. ukweli ni kwamba ili uweze kufanikiwa katika biashara ni vema ujue wateja unaowalenga ni kina nani. hii itakuwezesha kuuwapa huduma nzuri inayolenga mahitaji yao. kwa kufanya hivyo utaweza kuwa karibu zaidi na wateja wako na kuweza kukidhi mahitaji yao.
#4 KUWA NA MAZUNGUMZO YA KARIBU NA WAFANYAKAZI WAKO
Kuendesha biashara ni jambo gumu. Kwa kawaida kwenye mazingira ya kazi wafanyakazi kutokea kugombana, wengine hujikuta wakiwa hawaelewani kazini, wengine hufanya kazi kuliko wenzao na mambo kama hayo. Inakupasa wewe mwenye biashara kuwa muwazi unapo ongelea maswala ya biashara, na kuwahimiza wafanyakazi wako kuwa wawazi wakati wote.
Kuwa na utaratibu wa kuchukua maoni kutoka kwa wafanyakazi wako juu ya namna ya kuboresha utendaji kazi wa biashara yako. wazoeze wafanyakazi wako kutoa maoni. Na weka bayana kuwa hutotumia maoni yao kumlaumu awaye yeyote. Ukiwa na jambo la kusema sema kama lilivyo usijaribu kuficha ficha hii itakusaidia kuvuia ugomvi kazini.
#5 KUWA NA MATEGEMEO YANAYO WEZA KUFIKIKA
Kuendesha biashara ni jambo gumu, ukilinganisha na kuajiriwa. utajikuta ukihitajika kufanya kazi masaa mengi sana, ukifanya mambo usiyopenda na utakuwa na majukumu mengi sana kama kulipa mishahara nk. kwa upande mwingine unajenga jambo ambalo ni lako na lina kupatia uhuru wa kifedha. Kuwa na mategemeo yanayo weza kufikika itakusaidia kufurahia biashara yako.
Comments
Post a Comment