FURSA YA TANGAZA BIASHARA KUPITIA MTANDAO WA JAMII FACEBOOK
Katika
wavuti kuna fursa nyingi sana za kutangaza biashara kama kuweka matangazo
kwenye google, blogu mbalimbali zenye idadi kubwa ya wanaotembelea kwa siku,
kutumia mitandao mbali mbali ya jamii nk. Katika hizi, fursa kubwa zaidi ni ya
kutumia mtandao wa jamii Facebook.
Twakimu
zinaonesha kuwa Idadi ya watumiaji wa mtandao wa Facebook nchini ni watu
665,460 ambayo ni sawa asilimia 1.45 ya watanzania wote na asilimia 98.62 ya
watumiaji wa wavuti nchini.

Kati ya
hawa asilimia 71 ni wanaume na asilimia 29 ni wanawake.
Na idadi
kubwa ya watumiaji ni watanzania waliona umri kati ya miaka 18 hadi 35.
Kuna
faida nyingi za kutumia mtandao wa jamii facebook kutangaza biashara yako.
Faida hizi ni
- Utaweza kutangaza na kuwafikia wateja wako bure.
- Utawafikia wateja wako kwa urahisi na wakati,
- Utaweza kujenga mahusiano ya karibu na wateja wako
- Unafursa sawa na washindani wako ya kuweza kuwafikia wateja wako kwani biashara ndogondogo na kubwa zote zimepewa uwezo sawa wakutangaza biashara zao.
- Wateja wako wanakuwa na fursa ya kuweza kuwasiliana na wewe moja kwa moja na wewe kuwasiliana nao.
- Unaweza kupima na kujua idadi ya watu ulioweza kuwafikia kwa kutumia matangazo yako
- Unaweza kupanga na kuchagua ni watu gani unapenda ndo wafikiwe na matangazo yako.
Ili
kuweza kutumia kwa mafaniko mtandao wa jamii facebook kuwafikia wateja wako
zingatia mambo yafuatayo:
- Fahamu wateja wako(soko Lako) ni kina nani na je wapo katika mtandao wa jamii?
- Fanya utafiti kuweza kujua washindani wako wamechukua hatua gani katika kujitangaza kwenye mitandao ya jamii.
- Andaa timu ambayo itafanya shughuli ya kuuliza maswali kwa wateja na kujibu maswali ya wateja. Timu hii yaweza kuwa mtu mmoja, watu wawili au kadhaa, au wewe mwenye, hii ni kutokana na rasilimali watu uliyo nayo.
- Kuwa na malengo mahususi ya matangazo yako.
Je unataka kufanya nini?
- Watu waone tangazo?
- Watu wanunue bidhaa au huduma?
- Watu wapende na kujiunga na kurasa yako kwenye mtandao?
- Ukurasa wako kwenye mtandao lazima uwe na taarifa tofauti tofauti mpya kila siku au kila baada ya siku moja hivyo jiandae kwa taarifa utakazo kuwa unaweka.
- Hakikisha kuwa kila wakati unajua nini kinaendelea kwenye kurasa yako ilikuweza kusimamia comenti mbalimbali zinazokuja kutoka kwa watu. Hii itakuwezesha kusahili kama kuna jambo lolote linaloweza kuharibu jina la biashara yako.
Namna ya
kujitangaza Facebook.
- Tengeneza kurasa ya Facebook ambayo itakayo kuwa na taarifa za biashara yako.
- Anza kualika watu wapende na kujiunga na kurasa yako.
- Anza kuandika mambo mbalimbali yanayo vutia kwenye kurasa yako yaliyo na uhusiano na biashara yako
- Washirikishe wateja wako kwa kuuliza maswali, kuweka maswali ambayo watapiga kura nk.
- Unaweza pia kutengeneza tangazo dogo ambalo litakuwa linarushwa na Facebook kwenye secta yao ya matangazo mtu anapotembelea Facebook. Kwenye hili utachagua unataka tangazo lifikaje kutokana bugeti uliyonayo utalipia pale tu mpango wako umefikia malengo uliyoweka.
Kama huna
rasilimali watu ya kutosha kuweza kusimamia shughuli hii ya kutangaza kupitia
mitandao wa jamii kuna kampuni mbali mbali zinazo weza kufanya haya kuwa niaba
yako wewe ukawalipa kwa huduma yao.
Nakutakia
mafanikio mema unapoenda kuanza kutumia fursa hii kuwafikia wateja wako!



Comments
Post a Comment