MBINU MBALI MBALI ZA KUWEZA KUWEKA MAHUSIANAO MAZURI NA KUWAVUTIA WATEJA ILI WAENDELEE KUWA WATEJA WAKO.
Niliandika makala ya mambo muhimu katika biashara na jambo moja la muhimu nilisema ni kujua nani wateja wako. Mara nyingi tumekuwa tukipata wateja kwenye shughuli zetu za biashara lakini hatujaweka mipango ni namna gani tunaweza kuwavutia, kuwakumbusha kuhusu sisi na kuwafanya warudi tena kunua.Kuna mbinu mbali mbali unazoweza kutumia ili kuwa kumbusha wateja wako kuhusu huduma na bidhaa mbali mbali unazotoa.
# Kitabu cha kumbukumbu ya wateja
Tengeneza kitabu ambacho utaweka kumbukumbu ya wateja wako kama majina yao, namba za simu, walipotokea, tarehe zao za kuzaliwa, tarehe za kumbukumbu za ndoa au kuzaliwa kwa watoto wao na kadhalika kulingana na huduma au bidhaa unazouza. Tumia taarifa hizo kuendeleza mahusiano yenu mfano unaweza kuwatumia taarifa unapoleta bidhaa mpya au huduma. watumie salamu siku zao za kuzaliwa, za kumbukumbu za ndo au kuzaliwa kwa watoto wao na mambo kama hayo.Mimi kuna duka nilienda nikaacha taarifa zangu ambapo kila siku yangu ya kusherekea siku yangu ya kuzaliwa huwa wananitumia salamu, hii hunifanya nione wananithamini. huwa nawafikiria kila napotaka kununua bidhaa wanzo uza.
# Business card
Tengeneza business card zenye taarifa zako na huduma au bidhaa unazotoa. Unaweza weka chombo mezani mahali wateja wako wanapokuja kulipia bidhaa ama kupata huduma, weka business cards zako hapo wakija wachukue. Pia unapo maliza kuongea na mteja mkabidhi business card yako na mkaribishe tena kuja kununua bidhaa au huduma yako.# Vifungashio vyenye taarifa zako
Tengeneza mifuko mizuri yenye kuvutia ambayo itakuwa na taarifa zako. hakikisha ni mifuko ambayo akifika nayo anapokwenda atapendelea kuuhifhadhi atumie siku nyingine. Ni dhahiri kwamba atakapo tumia tena huo mfuko atakumbuka kuhusu bidhaa au huduma zako na huwenda akafikiria kupita kuona nini kipya.#kuponi mbali mbali
Unaweza kutengeneza kuponi ambazo wateja wako wakinunua bidhaa za thamani ya shilingi kadhaa unawapa kuponi ambazo wakirudi kununua tena bidhaa utawapa punguzo la asilimia kadhaa kulingana na unavyo ona wewe. kuponi hizo zitawakumbusha kuhusu biashara yako na pia kuwafanya watamani kuja ili kupata punguzo hilo la bei. Pia unaweza kuweka kuponi kwenye baadhi ya magazeti na makala mbali mbali zitolewazo bure amabazo wateja wako wanaweza kukata na wakija kununua bidhaa watapata punguzo fulani la bei.# Zawadi mbali mbali
Unaweza kuwa unabidhaa ndogo ndogo unazoweza kutoa kama zawadi kwa wateja wako wanapo nunua bidhaa kadhaa ua zenye thamani fulani. unaweza kuwapa zawadi moja kwa moja au kwa kutumia michezo mbali mbali itakayo pelekea wao kupata zawadi ya aina fulani. zawadi hizi huwenda zikawa ni bidhaa kama walizo nunua au vitu wanavyo weza kuwapelekea watoto wao au kuweka nyumbani kama urembo na kadhalika.
# Vipeperushi na broshua
Unaweza pia kutengeneza vipeperushi au broshua mbali mbali ambazo unaweza kuweka sehemu mbali mbali kama kwenye maduka, supermaketi, nk. hakikisha vinaelezea vizuri kuhusu bidhaa au huduma unazotoa, mawasiliano yako yaonekane vizuri na pia kama unaduka weka ramani ya jinsi ya kufika hapo.
Ni muhimu kuweka gharama ya kufanya mambo haya kwenye bugeti yako ya utafutaji masoko.
Je ni mbinu ipi nyingine unayo tumia wewe? niandikie hapo kwenye comments.




asante kwa fundisho lako umenisaidia sana
ReplyDeleteKaribu sana kuendelea kujifunza na kama una maswali niulize
Delete