KUWEKEZA KWA WAFANYAKAZI WAKO


Kuna mfanyabiashara mmoja maarufu nchini marekani aliyekuwa anamiliki viwanda, reli, meli nk jina lake ni Andrew carnegie  alisema kuwa; wakichukua mali zake zote, na biashara yake na kila alichonacho na kumwachia wafanyakazi wake  tu baada ya miaka kadhaa atarudi kuwa na utajiri ule ule aliyo kuwa nao mwanzo.

Unadhani ni kwanini alisema hivyo?

Andrew aliamini katika kuwekeza kwa wafanyakazi, aliwapa mafunzo mbali mbali na kuwaendeleza katika taaluma tofauti tofauti. Alijenga mahusiano mazuri na wafanyakazi wake ambayo yalipeleke kujengeka kwa imani kati yao na hivyo kupelekea kampuni yake kukua kwa kiwango cha juu sana  na yeye kuwa kati ya mabilionea nchi marekani na duniani kote.

Je wewe unawekeza kwa wafanyakazi wako?

Au ni baina ya wale wanotumia ujuzi wa wafanyakazi wao bila ya kuwaendeleza na pale wanapoona kuwa wanahitaji utaalamu mwingine zaidi ya ule waliyo nao wafanyakazi wao wanaenda kuajiri  wengine wenye utaalamu zaidi?

 Ukiwa kama mfanyabiashara naamini kuwa umekuwa ukipatwa na changamoto kubwa ya kupata wafanyakazi wazuri na kuweza kuwafanya wakae nawe kwa muda mrefu. Na kama wewe ni mfanyabishara  naamini unajua umuhimu wa kuwa na mfanyakazi mmoja wakumtegemea kwenye biashara yako.

Makampuni makubwa nchini kutumia mbinu hii ili kuhakikisha wanatoa huduma au bidhaa nzuri kwa wateja wao. Je si zaidi sana wewe uliye mdogo, wakati na unaye anza? Na huwenda makampuni hayo ni washindani wako.


Tafakari sasa na fanya mabadiliko!

  • Wape nafasi wafanyakazi wako ya kujiendeleza kitaaluuma, wengi hupendelea kujiunga na masomo ya jioni katika vyuo mbali mbali . Tengeneza mazingira ya kazi ambayo hayata mbana anaye soma.
  • Wapatie kozi fupi fupi ambazo unaamini zitawasaidia katika utendaji wao wa kazi. Kama cozi ya namna ya kukarimu wateja, namna ya kumhudumia mteja kwenye simu, namna ya kuelezea bidhaa au huduma unayotao kwa watu ilikumfanya mtu  kuwa mateja, na mambo kadha wa kadha
  • Wapatie zawadi mabali mbali kama bonas kwa wanaofanya kazi vizuri. Au pale mnapo pata ongezeko kubwa la faida.
  • Kwa anaye stahili ongezeko la mshahara kwa kazi anayo fanya mpatie hata kama ni ongezeko dogo tu litampa motisha ya kuendelea kufanya kazi vizuri.
  • Jenga mahusiano mazuri na wafanyakazi wako, ikibidii pata nafasi ya kuweza kuwafahamu na familia yake. Hii itakujengea ukaribu mzuri na hata kumfanya mfanyakazi wako kuona unamthamini.
  • Wahusishe wafanyakazi wako katika kupanga mipango mbali mbali ya biashara yako,mawazo yao ni ya muhimu sana. Katika hili utashangaa namna mawazo yao yanavyo weza kuwa natija kubwa kwenye biashara yako.
  • Usiwe na upendeleo wala kuweka madaraja kwa wafanya kazi wako, wathamini wote kwa kiwango sawa kwa kadiri uwezavyo.

Nakutakia mwanzo mzuri wa wiki na mafanikio makubwa katika kuwekeza kwa wafanyakazi wako na biashara yako.

Comments

Popular Posts